1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RSF wachukuwa udhibiti wa Kordofan Magharibi

31 Oktoba 2023

Wanamgambo wa kikosi cha Rapid Support Forces (RSF) nchini Sudan wametangaza kuwa wamechukua udhibiti wa uwanja wa ndege wa Belila uliopo jimbo la Kordofan Magharibi.

https://p.dw.com/p/4YDxH
Sudan | Mohamed Hamdan Daglo
Wanamgambo wa RSF wakiwa na kiongozi wao, Jenerali Mohamed Hamdan Daglo.Picha: Rapid Support Forces/AFP

Wafanyakazi katika kisima cha mafuta cha Belila, ambacho hutowa mapipa 10,000 hadi 12,000 kwa siku wamesema walihamishwa Jumapili usiku kutokana na mapigano hayo.

RSF imesema katika taarifa kuwa itaruhusu uwanja huo wa ndege na kisima cha mafuta kuendelea kufanya kazi.

Soma zaidi: MSF:Mashambulizi ya raia yamefikia kiwango cha kutisha Sudan

Mazungumzo yanayosimamiwa na Saudi Arabia kwa lengo la kupata makubaliano ya mpango wa kudumu wa kusitishwa mapigano yalianza upya Jumapili katika mji wa Saudia wa Jeddah.

Nalo Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu limesema liliusimamia mpango wa kuwachiwa maafisa 64 wa jeshi ambao walikuwa wamezuiliwa na vikosi vya RSF.