1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rome:Ujerumani kuisaidia Italy kuzuia wahamiaji haramu barani Ulaya.

28 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG39

Ujerumani imetuma polisi maalum wa mpakani ili kuisaidia Italy kushughulikia umiminikaji wa wahamiaji wasio halali kutoka Afrika wanaopitia katika kisiwa kidogo cha Lumpedusa.

Italy imekuwa ikilalamika kwa miaka kadhaa kwamba Ulaya ya Kaskazini haitoi msaada wa kutosha kuzuia umiminikaji wa wahamiaji wasio halali, wengi wahamiaji hao wakipitia katika visiwa vya Italy kwa kutumia boti za kihalifu.

Baadae wahamiaji hao wasio halali hujaribu kusafiri kuelekea nchini Ujerumani na mataifa mengine ya Ulaya, ambako tayari kuna familia zinazo wasubiri.