1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME : Rais Bashir wa Sudan yuko Italia

14 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBPv

Rais Omar Hassan al Bashir wa Sudan amewasili nchini Italia hapo jana kwa mkutano na viongozi wa nchi hiyo na Papa Benedikt wa 16 ziara ambayo nia ya aina yake Ulaya ya magharibi ambayo imezusha wasi wasi kutoka kwa watetezi wa haki za binaadamu na wanasiasa.

Al bashir atakuwa na mazungumzo mapema leo hii mjini Rome na Waziri Mkuu wa Italia Romano Prodi ambaye ameitetea ziara hiyo kuwa ni njia yenye manufaa kuishinikiza Sudan kutimiza ahadi zake kuhusiana na suala la Dafur.

Rais Bashir anawasili Italia ikiwa ni wiki chache kabla kuwekwa kwa kule kunakatogemewa kikosi cha kimataifa kulinda amani huko Dafur ambapo watu 200,000 wameuwawa na milioni mbili na nusu kupotezewa makaazi yao tokea kuzuka kwa mzozo kati ya waasi na serikali hapo mwaka 2003.