Rome. Prodi kupambana na Berlusconi katika uchaguzi.
18 Oktoba 2005Waziri mkuu wa zamani wa Italia Romano Prodi amepata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa awali unaomchangua mtu atakayeongoza upinzani katika nchi hiyo.
Prodi , rais wa zamani wa tume ya Ulaya , amepata asilimia 74 ya kura siku ya Jumapili, kwa mujibu wa matokeo kamili.
Viongozi wa muungano wa vyama vya mrengo wa kushoto kati, unaoundwa na takriban vyama tisa tofauti, wamekutana mjini Rome siku ya Jumatatu kuweza kufanya mapitio ya matokeo ya uchaguzi huo na kupanga mikakati yao katika uchaguzi wa bunge unaotarajiwa kufanyika mwakani.
Prodi sasa ataongoza muungano huo wa mrengo wa shoto katika uchaguzi huo, dhidi ya waziri mkuu wa sasa Silvio Berlusconi, katika juhudi za kurejesha wadhifa huo ambao aliushikilia katika miaka 1996 hadi 98.