1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rome. Kanisa katoliki limeanza siku tisa za maombolezo kutokana na kifo cha Papa.

9 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFOt

Kanisa Katoliki limeanza siku tisa za maombolezo kutokana na kifo cha kiongozi wa kanisa hilo Pope John Paul wa pili. Hii inakuja siku moja baada ya mazishi ya kiongozi huyo katika kanisa la St. Peters Basilica, mjini Rome. Zaidi ya viongozi 200 wa kisiasa na kidini pamoja na mamia kwa maelfu ya mahujaji walijazana katika uwanja wa St Peter katika eneo la Vatican kwa ajili ya mazishi ya Papa Paulo. Misa ya wafu iliyochukua saa tatu iliongozwa na Kadinali wa Kijerumani Joseph Ratzinger. Ndie kiongozi wa kundi la makadinali. Ujerumani iliwakilishwa katika mazishi hayo na ujumbe ulioongozwa na rais Horst Köhler na Kansela Gerhard Schröder. Kundi hilo la makadinali linakutana kwa siri kumchagua atakayechukua nafasi ya Yohana Paulo wa pili