1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Romania na Bulgaria zajiunga kwa sehemu katika Schengen

31 Machi 2024

Romania na Bulgaria zimejiunga na eneo la Schengen hii leo, ijapokuwa baadhi ya hatua za udhibiti wa mipaka zitaendelea kuwepo. Hii ina maana kuwa ukaguzi wa watu katika mipaka ya ndani ya angani na baharini.

https://p.dw.com/p/4eIBU
Uwanja wa ndege wa Henri Coanda mjini Otopeni, Romania
Raia wa Romania sasa wataweza kusafiri bila viza kuingia katika kanda ya Schengen barani UlayaPicha: Andreea Alexandru/AP Photo/picture alliance

Hii ina maana kuwa ukaguzi wa watu katika mipaka ya ndani ya angani na baharini, kwa maana ya viwanja vya ndege na bandari, hautafanyika tena.

Nchi za Umoja wa Ulaya zilikubaliana kuiongeza Bulgaria kwenye kanda ya Schengen mwishoni mwa mwaka wa 2023. Uamuzi wa kuondoa ukaguzi wa watu kwenye mipaka ya ardhini utachukuliwa baadaye kabla ya kukamilika kwa mwaka wa 2024.

Kanda ya Schengen ilianzishwa mwaka wa 1985 na inakusidia kuhakikisha uhamiaji huria wa watu zaidi ya milioni 400 barani Ulaya bila ukaguzi wa mipaka ya ndani.

Sasa linajumuisha 25 kati ya mataifa 27 wanachama pamoja na Iceland, Liechtenstein, Norway na Uswisi. Romania na Bulgaria zilikuwa zinasubiri kujiunga na Schengen tangu mwaka wa 2011. Rais wa Halmashauri Kuu ya Ulaya Ursula von der Leyen amepongeza mabadiliko hayo akiyaita kuwa ni mafanikio makubwa kwa nchi hizo mbili na kwamba ni tukio la kihistoria kwa eneo hilo kubwa zaidi ulimwenguni la kusafiri bila kibali.