ROMA: Vikosi vya Italia kuondoka Iraq
16 Machi 2005Matangazo
Waziri mkuu wa Italia,Silvio Berlusconi amesema nchi yake mwezi wa Septemba itaanza kuvirejesha nyumbani vikosi vyake vilivyokuwepo nchini Iraq.Alisema hayo muda mfupi baada ya wanasheria kupiga kura kuwabakisha wanajeshi 3,000 kwa miezi sita mingine nchini Iraq.Serikali ya Berlusconi mwezi Juni mwaka 2003,ilipeleka vikosi vyake kulinda amani,baada ya Marekani kuongoza uvamizi wa Iraq.Baada ya Marekani na Uingereza,Italia inachukua nafasi ya tatu kwa ukubwa wa vikosi vilivyopelekwa Iraq.