1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Roble aviagiza vikosi vya usalama kuchukua amri kutoka kwake

27 Desemba 2021

Waziri Mkuu wa Somalia amesema anaviamuru vikosi vyote vya usalama kuchukuwa amri moja kwa moja kutoka kwake na kuzua uwezekano wa kuongezeka kwa mvutano kati yake na rais Mohammed Abdullahi Mohammed al maarufu Farmajo.

https://p.dw.com/p/44sPp
Somalia Premierminister Mohamed Hussein Roble
Picha: Feisal Omar/REUTERS

Waziri Mkuu wa Somalia Mohamed Hussein Roble amesema leo kwamba anaviamuru vikosi vyote vya usalama kuchukuwa amri moja kwa moja kutoka kwake na kuzua uwezekano wa kuongezeka kwa mvutano kati yake na Rais Mohammed Abdullahi Mohammed al maarufu Farmajo.

Mapema leo, Roble alimshtumu raisi huyo kwa kupanga jaribio la mapinduzi. Katika taarifa iliyochapishwa katika mtandao wa Facebook wa shirika la habari la SONNA nchini humo, Roble amesema anataka kuwaambia watu wa Somalia kwamba hatua zilizochukuliwa na Farmajo ni jaribio wazi la mapinduzi dhidi ya serikali na katiba ya kitaifa.

Mvutano huo unaonekana kwa kiasi kikubwa kama juhudi za kuitatiza serikali kukabiliana na makundi ya waasi na umeifanya Marekani kutoa wito wa utulivu.