1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Robinson adai muwafaka wa kimataifa juu ya silaha ndogo:

18 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFiB
BOMBAY. Hapo jana mada kuu katika Mkutano wa Kimataifa wa Maswali ya Kijamii mjini Bombay, India, zilihusika na siasa mpya ya kiliberali katika sekta ya biashara na kilimo pamoja na kutolewa mwito wa kufanywa Mapatano ya UM juu ya Ukaguzi wa Silaha Ndogo. Aliyekuwa Kamishna wa UM wa Haki za Binadamu, Bibi Mary Robinson alisema kuwa silaha hizo ndogo kama bastola ndizo silaha za kuangamiza za enzi zetu. Kila mwaka wanauawa raiya wapatao 500,000 kupitia silaha hizo. Hasa hasa katika Kolumbia, Sierra Leone na Chechenia silaha hizo hutumiwa kukiuka haki za binadamu, alisema. Akasisitiza mwito wake kuwa hadi mwaka 2006 lazima ufikiwe Mkataba wa Kimataifa wa Ukaguzi wa Silaha Nsdogo.