1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RFK Jr asitisha kampeni ya urais, amuidhinisha Trump

24 Agosti 2024

Mgombea wa kujitegemea wa uchaguzi wa rais nchini Marekani Robert F. Kennedy Jr amesitisha kampeni yake na kumuidhinisha Mrepublican Donald Trump.

https://p.dw.com/p/4js3k
Marekani | Mgombea urais Robert F. Kennedy Jr. | 
RFK Jr. ni mtoto wa mgombea mtarajiwa wa urais Mdemocrat aliyeuawa Robert F. Kennedy Sr. na mpwa wa aliyekuwa Rais Mdemocrat John F. KennedyPicha: Thomas Machowicz/REUTERS

Hatua hiyo inahitimisha jaribio lake la kuingia Ikulu ya White House ambalo lilianzia katika chama cha Democratic. Kennedy amesema alikutana na Trump na washirika wake mara kadhaa na kugundua kuwa walikubaliana kuhusu masuala kama vile usalama wa mpakani, uhuru wa kujieleza na kumaliza vita.

Soma pia: Kamala Harris akubali rasmi uteuzi wa Democrat kuwa mgombea urais

Kennedy amesema ataondoa jina lake kutoka karatasi za kupigia kura katika majimbo 10 yenye mchuano mkali yanayoweza kuamua matokeo ya uchaguzi wa Novemba 5, na atabaki kuwa mgombea katika majimbo mengine. Watalaamu wa mikakati wanasema haijabainika kama uamuzi wa Kennedy utamsaidia Trump, ambaye yuko katika mchuano mkali na makamu wa rais Mdemocrat Kamala Harris.