1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Harris akubali rasmi uteuzi wa Democrat kugombea urais

23 Agosti 2024

Mgombea urais wa chama cha Democrat nchini Marekani Kamala Harris amekubali rasmi uteuzi wa chama chake kuwa mgombea wa urais.

https://p.dw.com/p/4jpGo
Marekani Chicago | Mgombea wa urais Kamala Harris
Kamala Harris, mgombea wa urais kupitia chama cha Democrat nchini MarekaniPicha: J. Scott Applewhite/dpa/AP/picture alliance

Harris amekubali uteuzi huo katika hotuba yake ya usiku wa jana, iliyokuwa siku ya nne na ya mwisho wa Kongamano la Kitaifa la chama cha Democrat.

Miongoni mwa mambo aliyozungumza ni pamoja na kuunga mkono hatua ya kusititisha vita vya Gaza na kuachiliwa kwa mateka wa Israel wanaoshikilia katika Ukanda wa Gaza. 

Mgombea huyo wa urais wa chama cha Democrat alitahadharisha juu ya madhara mabaya kwa nchi, iwapo Donald Trump atashinda uchaguzi wa urais wa Marekani wa mwezi Novemba.

Harris amewahimiza Wamarekani wasimchague Trump ambaye amesema anapanga kuongeza kodi tofauti na chama chake kinacholenga kupunguza mzigo wa kodi ili kuwanufaisha zaidi ya Wamarekani milioni 100.