1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripoti ya tume ya uchunguzi wa mto Mara yazua maoni mseto

Deo Kaji Makomba
21 Machi 2022

Wanaharakati wa mazingira na wanasiasa wametaka kuundwe tume huru itakayokuja na majibu sahihi kuhusiana na kuchafuka kwa mazingira ya mto Mara.

https://p.dw.com/p/48mkn
Dürre Hungersnot Afrika Flash-Galerie
Picha: picture alliance/dpa

Kwa mujibu wa taarifa ya uchunguzi wa kamati hiyo iliyokuwa chini ya mwenyeketi wake Profesa Samuel Manyele imeeleza kuwa, mto huo umeathiriwa kuanzia katika kijiji cha Marasibora wilayani Rorya na kijiji cha Wegero wilayani Butiama huku sababu ikielezwa ni kuwepo kwa kiwango kikubwa cha kinyesi cha mifugo mtoni pamoja na uozo wa mimea ndani ya mto hasa mimea vamizi kama vile magugu maji na matete na kwamba  mgodi wa dhahabu wa Barrick North Mara hauhusiki na uchafuzi huo.

Hata hivyo ripoti hiyo ya uchunguzi iliyotolewa Jumamosi iliyopita na kamati hiyo imeonekana kuwashangaza watu wengi nchini Tanzania na kuwaibua wanasiasa na wanaharakati wa mazingira huku wakihoji inawezekanaje kinyesi cha mifugo kama ng'ombe kusababisha uchafuzi wa mto Mara ulio kaskazini magharibi mwa Tanzania na kusababisha samaki ndani ya mto huo kufa na kuleta mashaka ya usalama wa watu wanaotumia maji ya Mto huo kwa matumizi mbalimbali ya kila siku.

Je, taarifa iliyotolewa imejaa siasa au uhalisia?

Tansania Plastikflaschen am Strand
Picha: Amas Eric in Dar es Salaam/DW

John Heche ni mkaazi wa wilayani Tarime mkoani Mara ambaye pia aliwahi kuwa mbunge wa jimbo la Tarime akizungumza na DW amesema kuwa sio kweli kwamba kinyesi cha ng'ombe kinaweza kusababisha uchafuzi wa mto huo na kwamba ripoti hiyo ni taarifa ya kejeli kwa wana Mara na Watanzania kwa ujumla na kuongeza kuwa.

Akisoma ripoti hiyo ya uchunguzi mjini Musoma mkoani Mara mwenyekiti wa kamati hiyo iliyoundwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Seleman Jafo, Profesa Samuel Manyele alimesema kuwa wamebaini uwepo wa kinyesi cha ng'ombe zaidi ya tani 1.8 milioni pamoja na mkojo wa ng'ombe lita 1.5 bilioni uchafu uliotokana na kuwepo kwa ng'ombe zaidi ya laki 3 waliokuwepo katika eneo oevu la mto Mara kwa kipindi cha miezi minane mwaka jana wakati wa kiangazi.

Hata hivyo ripoti hiyo imeonekana kutofautina na uchunguzi wa awali wa kimaabara uliofanywa na bonde la ziwa Victoria. Daktari Donald Kasongi ni mchambuzi na mwanaharaki wa mazingira akiwa jijini Mwanza Tanzania, anasema.

Mto Mara ni miongoni mwa mito mikubwa nchini Tanzania ambao hutirirsha maji yake kutokea kaskazini magharibi mwa nchi hiyo kuelekea ziwa Victoria huku ukitegemewa kwa matumizi mbalimbali na wakaazi wa maeneo jirani na mto huo ikiwemo uvuvi.