1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMali

OHCHR: Jeshi la Mali na wanajeshi wa kigeni wameuwa watu 500

12 Mei 2023

Jeshi la Mali na wapiganaji wa kigeni waliwauwa takriban watu 500 kwenye operesheni ya kupambana na wanamgambo wa itikadi kali katika eneo la katikati mwa Mali mnamo mwezi Marchi mwaka uliopita

https://p.dw.com/p/4RHjG
Mali | G5 Sahel Militärallianz
Picha: Hans Lucas/IMAGO

 Hayo yameelezwa katika ripoti iliyochapishwa leo na tume ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu, OHCHR. Tume hiyo imesema inaamini kwamba mauaji hayo yaliyotokea katika mji wa Moura yalifanywa kwa njia za ukiukaji sheria na misingi ya sheria ya kimataifa. Waliouwawa ni pamoja na wanawake 20 na watoto 7. Ripoti ya uchunguzi uliofanywa na kitengo kinachoshughulikia haki za binadamu katika ujumbe wa kulinda amani Mali, Minusma, imebaini kwamba jeshi la Mali na wanajeshi wa kigeni waliokuwa wamemaliza shughuli zao za doria katika eneo hilo ndio walioendesha mauaji hayo. Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk amesema yaliyobainishwa kwenye ripoti hiyo yanatisha.