1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripoti mpya inaonesha hatari kubwa ya njaa inaigubika Gaza

25 Juni 2024

Shirika linalofuatilia viwango vya njaa duniani, IPC, limesema Ukanda wa Gaza unaendelea kukumbwa na hatari kubwa ya njaa, wakati ambapo vita kati ya Israel na Hamas vikiendelea.

https://p.dw.com/p/4hVFU
Gaza/Rafah
Ripoti mpya inaonesha hatari kubwa ya njaa inaigubika GazaPicha: Mohammed Salem/REUTERS

IPC imesema katika tathmini yake mpya kuwa zaidi ya watu 495,000, sawa na zaidi ya humusi moja ya wakaazi wa Gaza, wanakabiliwa na viwango vikali zaidi, vya janga la ukosefu wa chakula.

Shirika hilo limesema kuongezeka kwa mgao wa ugavi wa chakula na huduma za lishe katika eneo la kaskazini mwa Gaza katika kipindi cha Machi na Aprili ulionekana kupunguza ukali wa njaa katika eneo hilo lililotabiriwa kukumbwa na viwago vikubwa vya njaa.

Mashambulizi ya Israel yawaua takribani 24 mjini Gaza

Lakini IPC imesema maboresho hayo yalioshuhudiwa mnamo mwezi Aprili yanaweza kufutika haraka.