1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Real Madrid yaipiku Barcelona na kunyakua ubingwa wa La Liga

Sekione Kitojo
20 Julai 2020

Mikono salama ya Zinedine Zidane kwa mara nyingine tena tangu kurejea Real Madrid aisaidia timu hiyo kunyakua  ubingwa  wa La Liga.

https://p.dw.com/p/3fbo1
Spanien Fußball La Liga Real Madrid Granada
Picha: picture-alliance/AP Photo/J. Breton

Msimu  wa  kandanda  wa  Uhispania ulimalizika  jana  Jumapili(19.07.2020) ambapo Real Madrid , Sevilla  na  Granada  zikiwa  miongoni  mwa washindi  wakubwa  na  Barcelona , Valencia na  Espanyol wakiwa washindwa wakubwa. Imeonekana  wazi kwamba  zile timu zilizofanya vibaya zaidi zilimtimua kocha angalau mmoja  katika msimu uliovurugika  kwa  miezi  kadhaa  kutokana  na  janga  la virusi  vya  corona na  kumalizika  bila ya  mashabiki.

Lionel Messi in Barcelona 2020
Mfungaji bora wa La Liga Lionel Messi 2020Picha: Imago Images/AFLOSPORT

Zinedine Zidane  ameiongoza  Real Madrid katika  ubingwa wake wa 34 wa  la  Liga  katika  siku  ya  mwisho  ya  msimu  kwa  ushindi  wa mabao 2-1 dhidi  ya  Villarreal. Karim Benzema  alifunga  mabao hayo  mawili  na  mabao yake  jumla  21 yalikuwa  muhimu  kwa  timu hiyo. Sergio ramos  amemaliza  wa  pili kwa  ufungaji  katika  klabu hiyo  msimu  huu  akiwa  na  mabao 12 na  huenda  Real wakampatia  mkataba  mwingine  kupindukia  2021  wakati  mkataba wake  wa  sasa  utakapomalizika.

Malaga vs. Real Madrid Jubel
Sergio Ramos wa Real MadridPicha: Reuters/J. Medina

Leonel Messi amepat  tuzo yake ya  saba  ya  ufungaji  mabao mengi  katika  La  Liga  jana  baada  ya  kupachika  mabao  mawili katika  kichapo cha  mabao 5-0 cha  Barcelona  dhidi  ya  Alaves katika  duru ya  mwisho.

Messi  amepachika  mabao 25, manne  zaidi  ya  Karim Benzema.