1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Real Madrid yaanza msimu na sare tasa

21 Septemba 2020

Real Madrid walianza safari ya kutetea taji lao la La Liga kwa sare tasa dhidi ya Real Sociedad. Ukosefu wa ubunifu katika safu ya mashambulizi uunaibua maswali kuhusu hatua zilizochukuliwa na klabu kabla ya kuanza msimu

https://p.dw.com/p/3inml
Champions League - Juventus v Olympique Lyonnais | Tor Memphis Depay
Picha: Reuters/P. Powel

kila mmoja alionekana kufurahi wakati Real Madrid ilifikia makubaliano ya kumtoa Gareth Bale kwenda Tottenham kwa mkopo wikiendi iliyopita. 

Lakini siku moja baada ya winga huyo wa Wales kuondoka, Real Madrid walianza safari ya kutetea taji lao la La Liga kwa sare tasa dhidi ya Real Sociedad jana. Ukosefu wa ubunifu katika safu ya mashambulizi uunaibua maswali kuhusu hatua zilizochukuliwa na klabu kabla ya kuanza msimu. Kocha Zinedine Zidane hata hivyo amepuuzilia mbali madai kuwa timu yake haionekani kuwa sawa msimu huu.

Mahasimu wa Madrid, Barcelona watasubiri hadi Jumapili ijayo kufungua msimu dhidi ya Villarreal huku macho yote yakiwa kwa Lionel Messi baada ya ombi lake la kutaka kuondoka na kisha akaamua kubaki. Mwingine aliyeamua kuondoka na akaondoka kweli ni Arturo Vidal ambaye leo amefanya vipimo vya kiafya nchini Italia kabla ya kukamilisha uhamisho wake na Inter Milan.