1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RANGOON: Miripuko imeuwa watu watatu nchini Burma

7 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFFf

Miripuko mitatu iliyotokea takriban kwa wakati mmoja katika mji mkuu wa Burma imeuwa si chini ya watu 3 na kuwajeruhi wengi wengine.Miripuko hiyo inayodhaniwa kuwa imesababishwa na mabomu ilitokea katika eneo lenye maduka mengi na kwenye kituo cha biashara mjini Rangoon.Usalama umeimarishwa katika mji huo baada ya shambulio kama hilo kutokea sokoni katika mji wa Mandalay siku 10 za nyuma.Katika shambulio hilo watu 2 waliuawa na wengine 15 walijeruhiwa.