1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RANGOON: Mashambulio yauwa watu 11 nchini Burma

8 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFFc

Miripuko minne katika mji mkuu wa Burma,Rangoon imeuwa si chini ya watu 11 na kuwajeruhi mia kadhaa wengine.Miripuko hiyo ililenga majengo yenye maduka ya kifahari na jengo la biashara.Serikali imevilaumu vikosi vitatu vya waasi wa kikabila na kikundi kimoja kinachopigania demokrasia kikiwa uhamishoni.Haya ni mashambulio yaliosababisha hasara kubwa sana tangu jeshi kunyakua madaraka miaka 40 iliyopita.Serikali ya kijeshi ya Burma kwa miongo kadhaa inapambana na vikosi vya kikabila vya wapiganaji wa chini kwa chini.