1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ramaphosa aapishwa

19 Juni 2024

Cyril Ramaphosa ameapishwa kwa muhula wa pili kama rais wa Afrika kusini leo katika hafla iliyofanyika mjini Pretoria.

https://p.dw.com/p/4hGYz
Cyril Ramaphosa
Rais Cyril Ramaphosa akiapishwa kuongoza kwa muhula mwengine nchini Afrika Kusini.Picha: Kim Ludbrook/EPA

Ramaphosa sasa anatarajiwa kuchagua baraza jipya la mawaziri katika serikali mpya ya muungano baada ya chama chake cha African National Congress (ANC) kupoteza wingi wake katika uchaguzi wa mwezi uliopita.

Soma zaidi: Ramaphosa kuapishwa kwa muhula mwengine Afrika Kusini

Alichaguliwa kama rais na wabunge Ijumaa iliyopita kwa kusaidiwa na chama kikuu cha upinzani na chama chengine kidogo cha tatu ambavyo vimeungana na ANC katika makubaliano ya muungano ya kuiongoza kwa pamoja nchi hiyo iliyostawi zaidi kiviwanda barani Afrika.

Marais wa sasa na wa zamani wa bara la Afrika ni miongoni mwa waliohudhuria kuapishwa kwa Ramaphosa katika kile kinachoonekana kuwa utakuwa muhula wa mwisho mgumu kwa rais huyo mpya wa Afrika Kusini.