1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH: Wito kukomesha mapigano kati ya Fatah na Hamas

19 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC0i

Rais wa Wapalestina,Mahmoud Abbas na Waziri Mkuu Ismail Haniya wametoa mwito wa kusitishwa mapigano kati ya makundi hasimu Hamas na Fatah. Hadi hivi sasa,juhudi zote za kutaka kukomesha umwagaji wa damu,hazikufanikiwa.Watu 54 wameuawa katika mapigano ya siku tano kati ya makundi hayo hasimu.Mapigano hayo yamehatarisha misingi ya serikali ya umoja wa kitaifa,iliyoundwa na makundi hayo mawili ya Wapalestina,miezi miwili iliyopita tu.