1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH: Uchaguzi wa bunge la Wapalestina umeahirishwa

4 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF76

Rais Mahmoud Abbas wa Wapalestina ameahirisha uchaguzi wa bunge uliotarajiwa kufanywa tarehe 17 mwezi wa Julai.Katika agizo lililotolewa,hakutaja tarehe mpya lakini amesema wakati zaidi unahitajiwa kusuluhisha mgogoro katika Baraza la kutunga sheria la Wapalestina kuhusika na mageuzi ya sheria ya uchaguzi.Kwa mujibu wa maafisa wa Kipalestina uchaguzi huenda ukafanywa mwezi wa Novemba.Waandishi habari wanasema hatua ya kuchelewesha uchaguzi inaweza kuzusha mvutano kati ya chama cha Fatah cha Abbas na Hamas kinachofuata siasa kali na ambacho hivi karibuni katika chaguzi za mabaraza ya miji kwenye Ukingo wa Magharibi na Gaza kilijinyakulia ushindi mkubwa.