1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ramallah: Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa aazungumza na Abu Mazen

14 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFX2

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan amekua na mazungumzo pamoja na kiongozi wa utawala wa ndani wa Palastina Mahamoud Abbas mjini Ramallah hii leo.Katibu mkuu Annan anaelitembelea kwa mara ya kwanza eneo la mashariki ya kati tangu miaka minne iliyopita, alitokea Jerusalem ambako alikutana na kuzungumza pia na waziri mkuu wa Israel Ariel Sharon.Akizungumza na waandishi habari,katibu mkuu wa Umoja wa mataifa amesema lengo la ziara hii ni kuupa msukumo utaratibu mpya wa amani ya mashariki ya kati ulioandaliwa kwa pamoja na Marekani,Umoja wa Mataifa,Umoja wa Ulaya na Rashia.Katibu mkuu Kofi Annan amesema jumuia ya kimataifa imepania kuona utaratibu wa amani unasonga mbele na kupelekea kuundwa haraka dola la Palastina.Kabla ya mazungumzo pamoja na rais wa Palastina,katibu mkuu Kofi Annan aliweka shada la mauwa juu ya kaburi la marehemu Yasser Arafat.Kesho katibu mkuu Annan atarejea Jerusalem ambako atahudhuria ufunguzi wa kumbusho jipya la wahanga wa mauwaji ya Holocaust-Jad Vachem.Kumbu kumbu hizo zitahudhuriwa pia na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Joschka Fischer,aliyeondoka Berlin kuelekea Israel.