1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH. Abbas asema wanamgambo wamepokonywa silaha.

20 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFLQ

Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas, amesema amefaulu kuwapokonya silaha wanamgambo wanaosakwa na Israel katika miji miwili ya ukingo wa magharibi. Akiwahutubia waandishi habari wa Israel katika makao yake makuu mjini Ramallah, Abbas alisema wanamgambo wote wa miji ya Jericho na Tulkarm, wamepokonywa silaha.

Abbas ameitoa taarifa hiyo kufuatia lawama za waziri mkuu wa Israel, Ariel Sharon, katika mkutano wa kilele na rais George W Bush wa Marekani, uliofanyika juma lililopita, kwamba Abbas ameshindwa kupambana na ugaidi katika mpango wa amani ya mashariki ya kati unaodhaminiwa na Marekani.