1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Rais Zelensky atarajia msaada zaidi wa ulinzi wa anga

9 Januari 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema mashambulizi makubwa ya hivi majuzi ya Urusi hayatoachwa bila kujibiwa na kusisitiza kuwa ni lazima Moscow ilipe uharibifu uliosababishwa na ugaidi.

https://p.dw.com/p/4b0K8
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akizungumza mjini Kyiv
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akizungumza na viongozi kadhaa wa Ulaya (wasioonekana pichana) katika mkutano wa pamoja mjini Kyiv: 23.11.2023Picha: AFP/Getty Images

Siku ya Jumatatu, Urusi ilifanya mashambulizi makali ya makombora katika miji ya Kryvyi Rih, Zaporizhzhia, Kharkiv, Dnipropetrovsk na Khmelnytskyi na kusababisha vifo vya watu wanne na kuwajeruhi wengine wapatao 45.

Zelensky amesema mazungumzo na washirika wake wa kimataifa katika miezi ijayo, yatalenga kuchukua hatua mbalimbali ili kuimarisha ulinzi wa anga wa Ukraine . Maafisa wa Urusi wamesema pia kuwa wamezuia mashambulizi kadhaa ya anga katika mji wao wa mpakani wa Belgorod.