1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSaudi Arabia

Rais Xi wa China kuanza ziara ya siku tatu Saudi Arabia

7 Desemba 2022

Rais wa China Xi Jinping anatarajiwa kuwasili leo mjini Riyadh kwa ziara ya siku tatu. Xi anapanga kukutana na viongozi wa Saudi Arabia, Ghuba na wa ulimwengu wa kiarabu.

https://p.dw.com/p/4KazL
China I Xi Jinping
Picha: Xie Huanchi/IMAGO

Ziara hiyo inayoanza leo jioni inatarajiwa kujumuisha mikutano kuanzia Alhamisi na Mfalme Salman, Mrithi wa Kiti cha Ufalme Mohammed, pamoja na mkutano wa kilele na viongozi wa Ghuba na Uarabuni.

Ziara ya Xi inajiri karibu miezi mitano baada ya Rais wa Marekani Joe Biden kuitembelea Saudi Arabia, na kuwaambia viongozi wa Kiarabu kuwa Washington haitaondoka na kuwacha ombwe la kujazwa na China, Urusi au Iran.

Nchi za Ghuba zimeimarisha mahusiano yao ya kiuchumi, kisiasa na usalama na China kwa miaka mingi sasa. China ni mshirika muhimu wa kibiashara wa Saudi Arabia na mteja wake mkubwa kabisa wa mafuta ghafi.