1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Rais Xi kuhudhuria mkutano wa BRICS Johannesburg

18 Agosti 2023

China imethibitisha kuwa Rais Xi Jinping atahudhuria mkutano wa kilele wa wiki ijayo wa mataifa ya BRICS huko Johannesburg.

https://p.dw.com/p/4VJYX
Xi ataongozana pamoja na mwenyeji wake, Rais Cyril Ramaphosa kwenye mkutano huo.
Xi ataongozana pamoja na mwenyeji wake, Rais Cyril Ramaphosa kwenye mkutano huo.Picha: Leah Millis/Pool/REUTERS

Wizara ya mambo ya nje ya China imesema Rais Xi Jinping atahudhuria mkutano wa kilele wa wiki ijayo wa mataifa ya BRICS huko Johannesburg na kisha baadaye atafanya ziara rasmi ya Afrika Kusini.

Msemaji wa wizara hiyo ya mambo ya nje, Hua Chunying, katika taarifa pia amesema, katika ziara hiyo itakayoanza tarehe 21 hadi 24, Xi ataongoza pamoja na mwenyeji wake, Rais Cyril Ramaphosa, mkutano wa China na Afrika.

Mamlaka za Afrika Kusini zinasema Rais Vladimir Putin ameamua kutohudhuria mkutano huo kutokana na waranti wa kukamatwa kwake uliotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ya ICC.

Hatua hiyo huenda ikaonekana kama ya aibu kwa Putin ambaye ndiye rais wa pekee katika kundi la nchi za BRICS ambaye hatohudhuria mkutano huo.

Nchi nyengine zilizoko katika kundi hilo ni Brazil, Urusi na India. Huu ndio mkutano wa kwanza wa ana kwa ana wa kundi hilo BRICS tangu mwaka 2019.