1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Xi aahidi kuisaidia Afrika kukuza viwanda vyake

Sylvia Mwehozi
25 Agosti 2023

Rais wa China, Xi Jinping amewaeleza viongozi wa Afrika kwamba nchi yake itazindua mipango ya kusaidia ukuaji wa sekta ya viwanda na kilimo barani afrika ili kuwa vya kisasa zaidi.

https://p.dw.com/p/4VYad
Rais Xi Jinping | BRICS
Rais wa China, Xi JinpingPicha: Sergei Bobylev/dpa/picture alliance

Rais wa China, Xi Jinping amewaeleza viongozi wa Afrika kwamba nchi yake itazindua mipango ya kusaidia ukuaji wa sekta ya viwanda na kilimo barani afrika ili kuwa vya kisasa zaidi. Xi, aliyasema hayo katika mazungumzo yake na viongozi na mawaziri kutoka Umoja wa Afrika, pembezoni mwa mkutano wa kilele wa kundi la nchi zenye kuinukia kiuchumi ulimwenguni, BRICS, ambao ulikamilika jana Afrika Kusini.

Rais huyo ameeleza kuwa China itatumia vyema rasilimali zake kwa ushirikiano na Afrika sambamba na mipango ya kibiashara katika kulisadia bara hilo kukuza sekta za viwanda na kilimo.

Mwanadiplomasia mkuu wa China kanda ya Afrika Wu Peng, alinukuliwa wiki hii akisema kwamba nchi hiyo inataka kubadili mwelekeo wake kutoka ujenzi wa miundombinu na kujielekeza zaidi katika kukuza viwanda vya ndani.