1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Zimbabwe aahidi uchaguzi wa "huru na haki"

19 Aprili 2023

Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ametoa ahadi ya kufanyika uchaguzi huru na wa haki kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu

https://p.dw.com/p/4QIBR
Glasgow | Präsident Emmerson Dambudzo Mnangagwa
Picha: Dominika Zarzycka/NurPhoto/picture alliance

Lakini pamoja na kauli hiyo aliyoitoa katika hotuba ya siku ya uhuru jana Jumanne, Mnangagwa pia alitoa onyo dhidi ya matendo ya asasi za kiraia alizoziita za kitapeli.

Taifa hilo la kusini mwa Afrika linatazamiwa kufanikisha uchaguzi wake wa urais na ubunge unaotarajiwa kufanyika mwezi Agosti, ingawa bado tarehe haijatangazwa.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 80, ambaye yupo katika jitihada ya kutaka kuchaguliwa tena, aliwataka Wazimbabwe kukataa ghasia, kabla, wakati na baada ya zoezi la upigaji kura.