1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaZimbabwe

Rais wa Zimbabwe kupambana na vigogo katika uchaguzi mkuu

22 Juni 2023

Rais wa Zimbabwe, kiongozi mkuu wa upinzani pamoja na kiongozi wa zamani wa chama tawala aliyekuwa uhamishoni kufuatia mapinduzi ni miongoni mwa watakaowania urais, katika uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi Agosti.

https://p.dw.com/p/4SvT6
Bildkombo Simbabwe Präsidentschaftswahlen Mnangagwa Chamisa
Picha: picture-alliance/AP Photo

Viongozi hao watatu tayari wamesajiliwa kugombea nafasi hiyo na tume ya taifa ya uchaguzi, ambayo inatarajia kutangaza orodha ya mwisho ya wagombea waliothibitishwa.

Rais Emmerson Mnangagwa wa chama tawala cha ZANU-PF anawania awamu ya mwisho na anatarajia kupata upinzani mkali kutoka kwa kiongozi wa upinzani Nelson Chamisa, aliyemshinda kwa umbali mdogo katika uchaguzi uliozozaniwa wa mwaka 2018.

Aliyewahi kuwa waziri kwenye serikali ya Robert Mugabe, Saviour Kasukuwere, aliyekimbilia uhamishoni nchini Afrika Kusini baada ya mapinduzi ya mwaka 2017, pia anawania nafasi hiyo, ingawa bado haijulikani kama tayari amerejea nchini humo.

 Uchaguzi huu wa Agosti unatarajiwa pia kufuatiliwa kwa karibu, katika taifa hilo lenye historia ya uchaguzi unaogubikwa na machafuko na mivutano.