1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Rais wa zamani wa Taiwan aitembelea China

27 Machi 2023

Rais wa zamani wa Taiwan Ma Ying-jeou ameanza hii leo ziara yake ya siku 12 nchini China na kuwa kiongozi wa kwanza wa Taiwan kuitembelea China ambayo inakataa kutambua uhuru wa kisiwa hicho kinachojitawala.

https://p.dw.com/p/4PIE5
Ma Ying-jeou
Picha: Arnulfo Franco/AP/picture alliance

Safari ya Ying-jeou mwenye umri wa miaka 73, inajiri wakati kukiwa na mvutano unaoongezeka kati ya China na Taiwan. Jana, Honduras ilivunja uhusiano na Taiwan na kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na China.

Mgogoro huo wa kidiplomasia umeripotiwa siku chache tu kabla ya ziara iliyopangwa ya Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen nchini Guatemala na Belize kuanzia Machi 29.

Chama tawala na baadhi ya vyama vya upinzani huko Taiwan vimeikosoa ziara hiyo Ma Ying-jeou, kwa hoja kwamba inapuuza ukweli kwamba China inaikandamiza Taiwan.