1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChile

Rais wa zamani wa Chile afariki katika ajali ya helikopta

7 Februari 2024

Rais wa zamani wa Chile Sebastián Piñera amefariki dunia hapo jana katika ajali ya helikopta.

https://p.dw.com/p/4c7Gh
 Rais wa zamani wa Chile - Sebastian Piñera
Rais wa zamani wa Chile Sebastián Piñera aliyefariki katika ajali ya helikoptaPicha: Esteban Felix/AP/dpa/picture alliance

Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo Carolina Tohá bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi kuhusu chanzo cha ajali iliyotokea katika mji wa kusini wa Lago Ranco.

Piñera aliyekuwa na umri wa miaka 74 aliiongoza  Chile  kwa mihula miwili kuanzia 2010 hadi 2014 na 2018 hadi 2022. Na utawala wake uligubikwa na matukio ya majanga ya asili ikiwa ni pamoja na tetemeko kubwa la ardhi lililofuatiwa na dhoruba iliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 500.

Viongozi mbalimbali wa Amerika Kusini akiwemo rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva na rais wa Argentina Javier Milei wametuma salamu za rambirambi wakimtaja kiongozi huyo kama mzalendo aliyekuwa na nia njema kwa taifa lake.