1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Ufaransa atoa shukrani kwa jimbo la Ujerumani

24 Aprili 2020

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amelishukuru jimbo la Ujerumani la North Rhine Westphalia kwa kuwapatia matibabu wagonjwa wa Kifaransa waliopata maambukizi ya virusi vya corona.

https://p.dw.com/p/3bMAK
Paris Präsident Macron
Picha: AFP/G. Fuentes

Katika barua aliyomtumia waziri mkuu wa jimbo hilo Armin Laschet na kuonekana na shirika la habari la dpa, Macron amesema wale waliopata maambukizi makali ya virusi hivyo waliweza kupewa huduma bora ya matibabu baada ya kusafirishwa nchini Ujerumani.

Mwishoni mwa mwezi Machi, wagonjwa wanane waliokuwa katika hali mbaya walisafirishwa kutoka mji wa Ufaransa wa Metz hadi mji wa Ujerumani wa Essen, ulio karibu na mpaka wa Ufaransa.

Mgonjwa mmoja aliyekuwa na umri wa miaka 76 alifariki dunia hospitalini Jumatatu iliyopita na wagonjwa wengine wawili walirudishwa Ufaransa baada ya kupata afueni. Wagonjwa zaidi wataendelea kutibiwa mjini Essen.

Chanzo: dpa