1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Tunisia amfuta kazi waziri wake wa nishati

5 Mei 2023

Ofisi ya Rais wa Tunisia, Kais Saied, inasema kiongozi huyo amemfukuza kazi Waziri wa Nishati Naila Nouira Al-Kenji.

https://p.dw.com/p/4QxSv
 Tunisian President Kais Saied
Picha: Johanna Geron/REUTERS

Hii ni mara ya pili kwa afisa wa serikali ya Tunisia kufutwa kazi ndani ya mwezi mmoja, baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani Tawfiq Charafeddine pia kuondolewa.

Hata hivyo, taarifa hiyo haikueleza sababu za kufukuzwa kazi Al-Kenji, na serikali ya Tunisia pia haijalizungumzia suala hilo.

Soma zaidi: Jaji nchini Tunisia aamuru kufungwa jela kiongozi wa upinzani Ghannouchi

Hatua hiyo huenda ikahusishwa na mzozo wa kisiasa na kiuchumi unaoendelea nchini humo.

Tunisia imekuwa ikikabiliwa na ghasia za kisiasa na kijamii tangu yalipofanyika mapinduzi ya mwaka 2011, na janga la COVID-19 limezidisha changamoto za kiuchumi.