1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Tanzania azindua mkutano wa mabunge wa SADC

Florence Majani3 Julai 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia S. Hassan, amezindua leo mkutano wa 53 wa Mabunge ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) pamoja na mambo mengine amezungumzia changamoto ya usalama wa chakula.

https://p.dw.com/p/4TMsS
Tansania Kamala Harris  Samia Suluhu Hassan
Picha: Ericky Boniphace/AP/picture alliance

Akizungumza katika Mkutano huo unaoyahusisha mabunge ya nchi 15 kati ya 16 wanachama wa SADC kwa wiki nzima, Rais Samia Suluhu Hassan amesema  nchi za SADC zina idadi ya watu milioni 380 na takribani asilimia 51.3 wanakabiliwa na njaa,. Amesema nchi hizo hazina budi kuweka mikakati ya kukabiliana na njaa.

" Tuna ardhi muhimu kwa ajili ya kilimo lakini tunapaswa kuhakikisha ardhi hii inazalisha chakula kuziba pengo linalofanya nchi za SADC kuwa na njaa,” amesema. Namna njema ya kufanikisha hilo, amesema ni utekelezaji wa sera mbalimbali na mikakati inayowekwa mara kwa mara kama ule wa mwaka 2015 wa SADC."

Soma pia: Mkutano wa Kilele wa SADC Kinshasa

Kadhalika Rais Samia amesema Kwa sasa kilimo kimekuwa chanzo kikuu cha ajira na kipato, kwa watu zaidi ya asilimia 61% ya watu katika nchi za SADC , hivyo serikali zetu zinatakiwa kutilia maanani sekta hii, ili kufikia malengo ya SADC ya 2050. Sadc ni miongoni mwa maeneo yenye idadi kubwa ya vijana, hivyo inatakiwa kutenegeneza ajira zaidi ya milioni 12 ili kuendana na mahitaji hayo.

Rais Samia apongezwa na viongozi wa SADC

Korruptionsbekämpfung in Angola
Picha: Borralho Ndomba/DW

Rais wa bunge la SADC Rogers Mancienne amempongeza Rais Samia:

"Kwa niaba ya forum, nampongeza kwa uongozi unaoonyesha imani kubwa katika kazi za mabunge ya jumuiya, nah ii naamini, inadhihihirsha imani yetu katika uwepo wa demokrasia."

Akizungumza katika mkutano huo, Spika wa Bunge la Tanzania, Dk Tulia Ackson amesema, nchi za SADC  zinaendelea kutimiza malengo yake ikiwamo kulinda demokrasia, utawala bora, usawa wa kijinsia na ulinzi wa haki za binadamu na akaongeza:

"Nchi za SADC hazitashindana lakini zitasaidiana nia ni kuhakikisha  kuna usalama wa chakula, ajira kwa vijana”

Kuhusu usawa wa jinsia, Rais Samia  amewataka viongozi wote kuendelea na jitihada na kupaza sauti zao kuhakikisha haki inatendeka. Mkutano huo umehudhuriwa na wabunge na maspika wa bunge wa nchi zaidi ya 15 za SADC na viongozi wa kitaifa wakiwamo mawaziri, wakuu wa mikoa.