1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTaiwan

Rais wa Taiwan akosoa mazoezi ya kijeshi ya China

11 Aprili 2023

Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen amesema mazoezi ya kijeshi ya China kukizunguuka kisiwa hicho yamesababisha kukosekana utulivu kwenye taifa lake na ukanda mzima na kukitaja kitendo hicho kuwa cha kutowajibika.

https://p.dw.com/p/4PtCh
Taiwans Präsidentin Tsai Ing-wen
Picha: Taiwan Presidential Office/AP/picture alliance

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Rais Tsai ameandika, kama rais anawakilisha taifa lake duniani na ziara zake nje ya nchi ikiwemo Marekani si jambo geni na kuongeza kwamba China ilitumia mwanya huo kuanzisha mazoezi ya kijeshi hatua ilioondoa utulivu kwa Taiwan na kanda kwa ujumla wake.

Matamshi hayo ameyatoa wakati China tayari imemaliza mazoezi yake ya kijeshi ya siku tatu yaliopewa jina la "Upanga wa Pamoja" ikiyataja yenye mafanikio makubwa.

China ambayo iliionya Marekani kumruhusu Tsai kukutana na Spika wa Bunge Kevin McCarthy  haijasita kufikiria kutumia nguvu kukirudisha Kisiwa hicho kinachojitawala kidemokrasia chini ya udhibiti wa Beijing.