1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Senegal ataka sheria ya msamaha itekelezwe mara moja

14 Machi 2024

Rais wa Senegal Macky Sall ameiambia serikali yake ianze kuitekeleza sheria ya msamaha mara tu itakapochapishwa rasmi. Sall ametoa amri hiyo huku kukiwa na matumaini ya kuachiwa kiongozi mkuu wa upinzani Ousmane Sonko

https://p.dw.com/p/4dWqa
Rais Sall wa Senegal
Rais wa Senegal Macky Sall Picha: Seyllou/AFP

Kulingana na taarifa ya baraza la mawaziri iliyotolewa jana, Sall ametoa amri hiyo huku kukiwa na matumaini ya kuachiwa kwa kiongozi mkuu wa upinzani, siku kumi kabla ya uchaguzi wa urais.

Katika harakati za kufikisha mwisho wiki kadhaa za mzozo baada ya kuahirisha uchaguzi uliokuwa ufanyike Februari 25, Sall alipendekeza muswada utakaosamehe vitendo vilivyohusika na maandamano ya kisiasa tangu mwaka 2021.

Wagombea urais Senegal waanza kampeini za uchaguzi

Sheria hiyo iliyopitishwa na wabunge wiki iliyopita inatarajiwa kuchapishwa hivi karibuni ila hakuna taarifa rasmi kuhusiana na lini itakapochapishwa.

Huenda wanasiasa wa upinzani waliofungwa jela Bassirou Diomaye Faye na Ousmane Sonko wakanufaika na sheria hiyo mpya.