1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Senegal ametangaza leo kuwa siku ya mapumziko

7 Februari 2022

Rais wa Senegal Macky Sall, ametangaza leo kuwa siku ya mapumziko nchini humo kusherehekea ushindi wa kwanza taifa hilo wa kombe la michuano ya soka ya mataifa ya Afrika AFCON.

https://p.dw.com/p/46ciU
AFCON Finale Senegal vs Ägypten
Picha: Charly Triballeau/Getty Images/AFP

Rais wa Senegal Macky Sall, ametangaza leo kuwa siku ya mapumziko nchini humo kusherehekea ushindi wa kwanza taifa hilo wa kombe la michuano ya soka ya mataifa ya Afrika AFCON.

Tangazo hilo, lilitolewa kupitia kituo cha televisheni kinachomilikiwa na serikali baada ya Senegal kuishinda Misri.

Rais Macky Sall aliyetarajiwa kuitembelea Comoros mwishoni wa wiki kushiriki mkutano ambao unazileta pamoja pia Misri na Ethiopia, aliifuta ziara yake ili kuikaribisha nyumbani timu yake mjini Dakar ikitokea Cameroon.

Timu ya taifa ya Senegal au Simba wa Teranga, waliongozwa na nyota wa klabu ya Uingereza ya  Liverpool ,Sadio Mane iliifunga  Misri iliyokuwa ikiongozwa pia na nyota wa Liverpool Mohammed Salah mabao 4-2 kupitia mikwaju ya penalti baada ya dakika 120 za mchezo.