1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Poland Andrzej Duda, aibuka kidedea uchaguzi wa rais

13 Julai 2020

Rais wa Poland Andrzej Duda ameibuka mshindi katika uchaguzi wa urais ulioandaliwa mwishoni mwa wiki. Uchaguzi huo ulikokuwa na ushindani mkali utamwezesha Duda kuongoza kwa muhula wa pili wa miaka mitano.

https://p.dw.com/p/3fE5Q
Polen I Präsidentschaftswahl I Andrzej Duda Sieger
Picha: AFP/J. Skarzynski

Kulingana na kura zinazokaribia kumalizwa kuhesabiwa, Duda alimshinda mpinzani wake wa karibu wa chama cha kiliberali aliyekuwa Meya wa Warsaw Rafal Trzaskowski.

Tume ya uchaguzi nchini Poland imesema kuwa Duda alipata asilimia 51.21 ya kura zilizohesabiwa kutoka maeneo asilimia 99.97. Mpinzani wake Rafal Trzaskowski alifuata nyuma kwa asilimia 48.79 ya kura hizo.

Mkuu wa tume hiyo ya uchaguzi Sylwester Marciniak, amesema matokeo ya mwisho rasmi yatatangazwa baadaye na kwamba huenda yakawa na tofauti kidogo lakini huku Duda akiwa na kura takriban nusu milioni Zaidi ya Trzaskowski katika kura zilizohesabiwa hapo awali, haitarajiwi kuwa kura zilizosalia zinaweza kubatilisha ushindi wa Duda .

Kura hiyo iliyokuwa na ushindani mkali ilionesha mgawanyiko mkubwa wa tamaduni katika taifa hilo la Umoja wa Ulaya.

Polen Stichwahl Präsidentenamt | Rafal Trzaskowski
Rafal Trzaskowski aliyekuwa mpinzani wa Duda uchaguzi wa raisPicha: Getty Images/O. Marques

Uchaguzi huo ulifuatia kampeini kali iliyoghubikwa na masuala ya tamaduni ambapo shirika la habari la serikali na kanisa katoliki lenye ushawishi mkubwa nchini humo, zilitafuta uungwaji mkono wa Duda anayezingatia udumishaji wa masuala ya kijamii na kuongeza hofu ya wayahudi, jamii ya mashoga na wasagaji na wajerumani.

Duda anayeungwa mkono na chama tawala kinachoegemea siasa za mrengo wa kulia cha sharia na haki, alifanya kampeini yake kwa kuangazia maadili ya kitamaduni na kuoanua sera maarufu za matumizi ya umma katika taifa hilo la kikatoliki.

Sera za chama cha Duda zinazojumuisha marupurupu ya dola 125 kwa kila mtoto katika familia bila ya kujali mapato ya familia , zimesaidia kuondoa umaskini katika maeneo ya mashambani na kuzipa familia pesa Zaidi za matumizi.

Duda pia alikuwa na uungwaji mkono wa wazee nchini humo baada ya yeye na chama chake kushukisha miaka ya kustaafu na kuanzisha marupurupu ya kila mwaka ya pesa yanayojulikana kama pensheni ya 13.

Wafuasi wa Duda walimsifu pamoja na chama chake kwa kutoa ahadi nzuri za kupunguza ukosefu wa usawa kiuchumi hatua ulikuja na mabadiliko ya nchi kutoka kwa mfumo wa kikomunisti hadi wa uchumi wa masoko miongo mitatu iliyopita.

Lakini chama hicho pia kilichochea mzozo na Umoja wa Ulaya kutokana na sharia ambazo zimekipa nguvu Zaidi juu ya mahakama za juu na taasisi za sharia.

Polen Warschau Präsidentschaftswahl
Wapiga kura wa Poland mara baada ya kupiga kura siku ya JumapiliPicha: Reuters/A. Szmigiel

Viongozi wake wametumia matamshi ya ubaguzi dhidi ya jamii ya mashoga na wasagaji na makundi mengine madogo na chama hicho kimegeuza televisheni ya kitaifa kama chombo cha kueneza uvumi wakati wa kampeini za Duda na kumharibia sifa Trzaskowski.

Uchaguzi huo wa jumapili ulipangiwa mwezi Mei lakini ukacheleweshwa huku kukiwa na mzozo mkali wa kisiasa.

Trzaskowski aliyekuwa mbunge wa bunge la Ulaya aliyejiingiza katika kinyanganyiro hicho kuchelewa, aliapa kulinda haki za kidemokrasia za nchi hiyo na kuunganisha jamii iliyogawanyika huku akidumisha sera maarufu za maslahi.
Trzaskowski, alitia saini azimio la kuwavumilia mashoga na wasagaji hatua iliyochochea shtuma kali kote nchini humo. Mara kwa mara chama tawala kimepinga kuhusu haki za mashoga na wasagaji na kusema ni mienendo ya kutoka nje inayotishia kitambulisho cha Poland.