1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Nigeria atuma vikosi vya jeshi kuwaokoa wanafunzi

8 Machi 2024

Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu leo amepeleka vikosi vya majeshi kuwaokoa zaidi ya wanafunzi 250 waliotekwa nyara na watu waliojihami kwa bunduki kutoka shule moja kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4dJuR
Nigeria | Wahlen Bola Tinubu
Rais Bola Tinubu wa NigeriaPicha: Ben Curtis/AP Photo/picture alliance

Tukio hilo ni mojawapo ya matukio makubwa zaidi ya utekaji nyara kuwahi kutokea nchini humo katika kipindi cha miaka mitatu. Na sasa Rais Tinubu anasema ana imani kwamba wahanga wa tukio hilo wataokolewa na kwamba haki itapatikana. Tukio hilo na lile kubwa la utekaji nyara lililotokea wiki iliyopita katika jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa Nigeria, katika kambi ya watu walioachwa bila makao kutokana na machafuko yanayosababishwa na wanamgambo wa kijihadi, yanaashiria changamoto anayokabiliwa nayo Tinubu aliyeahidi kuifanya Nigeria kuwa salama na kuleta misaada zaidi ya kigeni.