1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndia

Rais wa Marekani Biden awasili India kwa mkutano wa G20

8 Septemba 2023

Rais wa Marekani Joe Biden amewasili India leo Ijumaa tayari kwa mkutano wa kilele wa nchi 20 tajiri zaidi ulimwenguni.

https://p.dw.com/p/4W7yj
Vor dem G20-Gipfel in Indien | Joe Biden, Präsident der USA
Picha: Evan Vucci/AP/dpa/picture alliance

Kufuatia hatua ya Rais Vladimir Putin wa Urusi na Rais Xi Jinping wa China kutohudhuria, Biden anatumai kutumia fursa hiyo kuongeza ushawishi wa nchi yake.

Kulingana na taarifa kutoka Ikulu yake White House, baada ya kuwasili, Biden anatarajiwa kukutana na waziri mkuu wa India Narendra Modi na atazungumza pia na viongozi wengine pembezoni.

Katika tukio jingine, rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Charles Michel  amesema Umoja wa Afrika uko mbioni kujiunga na kundi la nchi zenye uchumi mkubwa wa viwanda ulimwenguni G20.

Michel amesema makubaliano miongoni mwa  wanachama wa G20  kuujumuisha Umoja wa Afrika yalikuwa ishara nzuri. Haijabainika waziwazi ni lini umoja wa Afrika utakuwa mwanachama rasmi wa G20.