1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kusini

Rais wa Korea Kusini afanya ziara nchini Ukraine

15 Julai 2023

Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol amefanya ziara nchini Ukraine leo ambapo anakutana kwa mazungumzo na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.

https://p.dw.com/p/4Twfb
Südkorea Präsident Yoon Suk-yeol
Picha: Foto Olimpik/NurPhoto/IMAGO

Ziara hiyo ya kushtukiza imetangazwa leo na ofisi ya rais ya Korea Kusini na imefanyika baada ya Rais  Yoon kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya kujihami ya NATO wa wiki iliyopita. Katika mkutano huo Yoon alionesha mshikamano na Ukraine na kutafuta njia za kuisaidia kwenye mapambano dhidi ya uvamizi wa Urusi.

Korea Kusini yajiandaa kuipelekea Kyiv vifaa vya kutegua mabomu 

Mapema wiki hii, Rais huyo wa Korea Kusini alisema kuwa serikali yake ilikuwa ikijiandaa kuipelekea Kyiv vifaa vya kutegua mabomu yaliyotegwa ardhini na magari ya kubebea wagonjwa baada ya kuombwa na Ukraine. Awali wawili hao walipokutana mwezi Mei, Zelensky alimuomba Yoon kuongeza msaada wa kijeshi.