1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaVisiwa vya Comoros

Rais wa Kongo afanya mazungumzo na kiongozi wa Komoro

10 Februari 2023

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kogo Felix Tshisekedi amelaani kile alichokiita vita vya kinyama vinavyoendelea mashariki mwa nchi yake.

https://p.dw.com/p/4NK2B
Felix Tshisekedi | Präsident Demokratische Republik Kongo
Picha: Arsene Mpiana/AFP/Getty Images

Tshisekedi aliyasema hayo Alhamisi wakati wa ziara yake katika Visiwa vya Komoro.

Rais huyo wa Kongo alifanya mazungumzo na mwenzake wa Komoro Azali Assoumani, anayepigiwa upatu kuchukua urais wa kupokezana wa Umoja wa Afrika kutoka kwa Senegal wiki ijayo.

Tshisekedi alimwambia Assoumani kuwa kila sehemu anayokwenda, amekuwa akizungumzia vita vya kinyama vinavyofanywa na Rwanda nchini Kongo.

Tshisekedi pia alikuwa nchini Angola mapema wiki hii kwa mazungumzo na Rais Joao Lourenco, ambaye ni mpatanishi wa Umoja wa Afrika kati ya Kongo na Rwanda katika mzozo unaotokota mashariki mwa Kongo.