1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Iran asema ataiunga mkono kundi la Hamas

11 Julai 2024

Rais mteule wa Iran, Masoud Pezeshkian amelihakikishia kundi la wapiganaji wa Kipalestina la Hamas, uungaji mkono wa nchi yake, hayo ameyaeleza katika barua aliyomwandikia kiongozi wa Hamas, Ismail Haniyeh.

https://p.dw.com/p/4iBdz
Tehran, ran | Rais mteule Masoud Pezeshkian
Rais mteule wa Iran, Masoud Pezeshkian akipiga picha na baadhi ya Wairan.Picha: Vahid Salemi/AP/picture alliance

Pezeshkian amesema Iran itaendelea kuwaunga mkono kikamilifu watu wanaokandamizwa wa Palestina hadi yatakapotekelezwa madai yao halali na kukombolewa kwa mji wa Jerusalem. 

Katika barua hiyo Pezeshkian ameishutumu Israel kwa kufuata sera za ubaguzi wa rangi na kusema ni wajibu wa kibinadamu na Kiislamu kushirikiana na watu wa Palestina kukomesha kabisa sera hiyo mara moja. 

Soma pia:Masoud Pezeshkian: Nini cha kutarajia kutoka kwa rais mpya wa Iran

Siku ya Jumatatu, Pezeshkian alithibitisha katika taarifa yake kwa kiongozi wa kundi la Hezbollah la Lebanon, Hassan Nasrallah kwamba ataendelea kufuata mkondo wa Iran kuipinga Israel.