1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Xi Jinping kuzungumza na viongozi wa kiarabu mjini Beijing

29 Mei 2024

China imewakaribisha hii leo viongozi wa juu pamoja na wanadiplomasia kutoka mataifa ya kiarabu kabla ya mkutano ulioitishwa na Beijing unaolenga kuimarisha mahusiano kati ya nchi hiyo na Kanda ya mataifa ya kiarabu.

https://p.dw.com/p/4gPmW
 Xi Jinping na Mohammed bin Salman
Rais wa China Xi Jinping akíwa na mwenzake wa Saudi Arabia Mwanamfalme Mohammed Bin Salman Picha: Royal Court of Saudi Arabia/AA/picture alliance

Miongoni mwa viongozi wa juu watakaoshiriki mkutano huo ni pamoja na rais wa Misri Abdel Fattah al Sisi na rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan pamoja na viongozi wengine wa kikanda na wanadiplomasia. 

Rais Xi Jinping anatarajiwa kutowa hotuba yake  muhimu kesho Alhamisi atakapofunguwa mkutano huo unaolenga kupata msimamo wa pamoja  kati ya China na nchi za Kiarabu. 

Saudi Arabia yalaani mashambulizi ya Israel huko Rafah

Ajenda kuu ya mkutano huo ni  vita kati ya kundi la wanamgambo la Hamas na Israel, ambapo rais huyo wa China ametowa mwito wa kufanyika  mkutano wa kimataifa wa amani kuutatua mgogoro huo.

Kihistoria China imekuwa ikiunga mkono Palestina pamoja na mwelekeo wa kutaka suluhisho la kuundwa  madola mawili,kumaliza mgogoro kati ya Israel na Palestina.