1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Benki ya Dunia atangaza kujiuzulu

16 Februari 2023

Rais wa Benki ya Dunia David Malpass ametangaza kujiuzulu mwishoni mwa mwezi Juni.

https://p.dw.com/p/4NZk8
Weltbankpräsident David Malpass
Picha: ANDREW KELLY/REUTERS

Kwenye tangazo hili la ghafla, Malpass amesema ataachia ngazi ifikapo Juni 30 baada ya kuiongoza taasisi hiyo kwa zaidi ya miaka minne, hii ikiwa ni kulingana na taarifa ya Benki hiyo yenye makao yake makuu mjini Washington.

Soma pia:Benki ya Dunia yatoa dola milioni 250 kutwaa silaha za waasi Congo

Malpass anaondoka mwaka mmoja kabla ya muda wake kumalizika na katika kipindi cha uongozi wake, amejikuta akikabiliwa na ukosoaji mkalikutokana na matamshi yake ya kutokukubaliana na mgogoro unaosababishwa na athari za mabadiliko ya tabianchi.