1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKyrgyzstan

Rais Vladimir Putin awasili nchini Kyrgyzstan

12 Oktoba 2023

Rais wa Urusi Vladimir Putin amewasili nchini Kyrgyzstan Alhamisi kwa ziara yake ya kwanza ya kigeni tangu kutolewa kwa waranti wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC dhidi yake mwezi Machi.

https://p.dw.com/p/4XRRf
Ziara ya Putin nchini Kyrgyzstan ni ya kwanza kwa mwaka 2023 tangu kutolewa kwa waranti dhidi yake wa ICC. Oktoba 12, 2023.
Ziara ya Putin nchini Kyrgyzstan ni ya kwanza kwa mwaka 2023 tangu kutolewa kwa waranti dhidi yake wa ICC. Oktoba 12, 2023.Picha: ERGESH ZHUSUBALIEV/AFP

Kwenye ziara hiyo ya siku mbili, Putin anatarajkiwa kukutana na rais Sadry Zhaparov na kuhudhuria mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Madola Huru, CIS, iliyoundwa baada ya kuanguka kwa uliokuwa Muungano wa Kisovieti.

Putin analenga kuimarisha ushawishi endelevu wa Urusi katika eneo la Asia ya Kati kama ilivyo kwa mataifa mengine yenye nguvu ya China, Marekani na Umoja wa Ulaya katika eneo hilo la kimakakati kati ya Ulaya na Asia.

Hii ni ziara ya kwanza ya Putin kwa mwaka huu tangu kutolewa kwa waranti huo wa ICC baada ya kuivamia Ukraine Februari 2022 na kumtuhumu kwa matukio kama ya utekaji na kuwaondosha watoto kwenye maeneo yanayokaliwa na Urusi nchini Ukraine.