1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Tshisekedi aidhinisha dola mil. 10 kukabiliana na mpox

23 Agosti 2024

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi ameidhinisha kwa mara ya kwanza kiasi cha dola milioni 10 za Kimarekani ili kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Mpox.

https://p.dw.com/p/4jrUz
Virusi vya mpox hivi sasa vimefika katika maeneo mbalimbali ulimwenguni
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeanza kuchukua hatua za kukabiliana na maambukizi makubwa ya mpox nchini humoPicha: Dado Ruvic/REUTERS

Kongo imeripoti zaidi ya visa vipya 1,000 vya ugonjwa wa Mpox katika kipindi cha wiki moja iliyopita. Mamlaka za afya za Afrika zimeomba chanjo zinazohitajika kwa haraka kusaidia kupambana na tishio la Mpox linaloongezeka katika bara hilo.

Wakati huo huo Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO, limesema washirika wake kama vile Gavi na Unicef ​​wanaweza kuanza kununua chanjo ya mpox kabla ya kuidhinishwa na Umoja wa Mataifa.

Hatua hiyo inakusudia kuharakisha chanjo hiyo barani Afrika kupambana na mlipuko wa Mpox. Baadhi ya chanjo za Mpox zilizotolewa zinatarajiwa kuwasili Afrika wiki ijayo.