1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Samia ataka chama cha CCM kuendana na mabadiliko

Deo Kaji Makomba
1 Aprili 2022

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Chama chake cha CCM lazima kiendane na mabadiliko ya siasa za dunia zinavyokwenda na bila kufanya hivyo chama hicho kitashindwa kusonga mbele.

https://p.dw.com/p/49Lnx
EAC Staaten Video-Konferenz | Samia Suluhu Hassan
Picha: Philbert Rweyemamu/EAC

Rais Samia ameyasema hayo hii leo jijini Dodoma wakati wa mkutano mkuu maalumu wa chama hicho kilichompitisha kwa kura za kishindo makamu mwenyekiti wake mpya Abdulaman Kinana. 

CCM kutathmini marekebisho ya enzi za Hayati Magufuli

Chama tawala cha Tanzania chaanza vikao vya awali

Akizungumza katika hadhara ya wajumbe wa mkutano mkuu huo maalumu wa CCM Rais Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni mwenyekiti wa chama hicho amesema kuwa kuna mabadiliko ya mifumo ya siasa ndani ya dunia na ndani ya Tanzania kwa msingi huo lazima CCM ibadilike kwendana na siasa zinavyobadilika vinginevyo watashindwa kwendana na mabadiliko hayo.

Aidha Rais Samia amesema kuwa mabadiliko yanayofanywa na CCM hivi sasa ni kwa ajili ya kwendana na mabadiliko ya mifumo ya siasa.
Aidha Rais Samia amesema kuwa mabadiliko yanayofanywa na CCM hivi sasa ni kwa ajili ya kwendana na mabadiliko ya mifumo ya siasa.Picha: picture-alliance/AP Photo

Kwa upande wake makamu mwenyekiti mpya wa CCM Abdulhaman Kinana akizungumza mara baada ya kuidhinishwa kwa kura za wajumbe wote kushika nafasi ya makaumu mwenyekiti wa chama hicho amesema kuwa hakuna chama cha mtu isipokuwa kuna chama cha CCM na kwamba ndani ya CCM hakuna ukanda, ukabila wala udini na kwamba ni miongoni mwa mambo atakayoyavalia njuga ili kuondoa chembechembe hizo.

Kinana ambaye aliwahi kuwa Katibu mkuu wa chama hicho lakini pia akishika nafasi mbalimbali ndani ya chama na serikali ameongeza kusema kuwa wana CCM wanaweza kutofautiana kwa hoja na sio vinginevyo. Kadharika amesema kuwa kazi yake ya kwanza ni kukiimarisha chama kiwe chama imara kinachokubalika na kuheshimika miongoni mwa watanzania na akagusia suala la demokrasia ndani ya CCM.

Kinana achaguliwa makamu mwenyekiti wa CCM kwa kishindo