1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Ramaphosa hatimaye ateua baraza jipya la mawaziri

1 Julai 2024

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametangaza baraza jipya la mawaziri huku vyama vya zamani vya upinzani vikijizolea nafasi 12 kati ya 32 za uwaziri.

https://p.dw.com/p/4hhuQ
Südafrika Kapstadt | Cyril Ramaphosa und John Steenhuisen
Kiongozi wa DA John Steenhuisen na Rais RamaphosaPicha: South African GCIS/AP/picture alliance

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametangaza baraza jipya la mawaziri huku vyama vya zamani vya upinzani vikijizolea nafasi 12 kati ya 32 za uwaziri.

Chama tawala cha African National Congress ANC ambacho kimetawala nchi hiyo kwa miaka 30, kimebaki na nafasi 20 kati ya hizo, zikijumuisha wizara muhimu za mambo ya kigeni, fedha, ulinzi, sheria na polisi. Ramaphosa asema bunge Afrika Kusini kufunguliwa Julai 18

Chama kikuu katika ushirika wa serikali ya Umoja wa Kitaifa cha Democratic Alliance DA, kitashikilia nafasi 6 za mambo ya ndani, mazingira na huduma za umma. Kiongozi wake John Steenhuisen ameteuliwa kuwa waziri wa kilimo.

Vyama vingine vidogo katika serikali hiyo pia vimeshuhudia viongozi wake wakipewa nafasi za uwaziri. Kwa miongo kadhaa ANC imejivunia kukomesha ubaguzi wa rangi, lakini wapiga kura walikasirishwa na rekodi yake mbaya katika kushughilikia huduma za msingi.