1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Putin asifu Umoja wa Ulaya

10 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFEq

Mosko:

Rais Vladimir Putin wa Urussi leo amesifu mapatano yaliyofikiwa ya kushirikiana zaidi kisiasa na kiuchumi na Umoja wa Ulaya. Amesema kuwa hiyo ni hatua kubwa itakayoanzisha Ulaya isiyokuwa na vizuizi. Urussi na Umoja wa Ulaya zimetia saini mkataba wa kushirikiana zaidi katika nyanja nne ambazo ni ulinzi wa nje na ndani, uchumi, sayansi na utamaduni. Mapatano hayo yametiwa saini na Rais Putin na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya, José Manuel Barroso na Mwenyekiti wa Baraza la Umoja wa Ulaya, Waziri Mkuu wa Luxembourg, Jean-Claude Juncker. Rais Putin akifungua mkutano mkuu wa Viongozi mjini Mosko amesema kuwa mwenendo wa kuanzisha Ulaya kubwa baada ya ukuta wa Berlin kuanguka bado unaendelea. Anataka Ulaya isiyokuwa na mipaka.